
Muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mzee Edwin Mtei
amemsifu Rais John Magufuli kwa kazi yake ikiwa ni muda mfupi tangu
aingie madarakani. Mzee Mtei ambaye pia ni Gavana wa kwanza wa Benki Kuu
ya Tanzania, amesema kuwa Rais Magufuli ni mtu ambaye anaonesha shauku
ya maendeleo. Aliongeza kuwa endapo Rais Magufuli ataendelea kuishi kile
anachokisema, anaamini atasimamia vizuri ukuaji wa uchumi wa nchi.