WAZIRI wa
Mambo Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema njia ya kudhibiti dawa za
kulevya kuingia nchini ni kuweka mfumo wa kisasa wa kudhibiti uingiaji
dawa hizo, kuwa na orodha ya waingizaji wa dawa ni kazi bure kutokana na
kukosa mamlaka ya kisheria.
Kitwanga
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Maafisa
Wakuu wa Jeshi la Polisi, amesema katika kukabiliana na uingizaji wa
dawa za kulevya ni kuweka mfumo imara na jeshi la polisi lazima
lijipange katika udhibiti huo.
Kitwanga
amesema kuwa mfumo wa kiteknolijia ukiwekwa hautabagua mtu yeyote au
mkubwa katika madaraka awe mdogo wakishajulikana watachukuliwa hatua za
kisheria bila kuangaliwa nafasi walizo nazo.
“Orodha
ya wauza unga ukiwanayo haitasaidia na kufanya hivyo ni kuhisi, lakini
huna sheria ya kuweza kuwabana katika orodha hiyo” amesema Kitwanga.Kitwanga
amesema kuwa katika mambo waliyojpanga nayo na jeshi la polis ni
kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika bandari ili kuweza kudhibiti
utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.
Hata
hivyo amewataka polisi watu washitakiwe kwa kesi walizo nazo na sio
kuwabambikia watu wasio na hatia kusababisha kufungwa kwa kesi
zisizowahusu.
Kitwanga
amesema utoroshaji wa madini,jeshi la polisi haliwahusu wakihitajika na
Wizara ya Nishati na Madini watafanya hivyo katika kukabiliana na
utoshaji huo.
Aidha
amesema kati ya askari 45,000 ni askari 10,000 ndio wenye makazi hivyo
wanatarajia kujenga nyumba 5000 ikiwa nia nia askari wote kukaa katika
makambi ni rahisi kuweza kuhitajika kwa muda wowote.