Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars),
Rogasian Kaijage amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo baada ya kuomba kwa
uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).
Kaijage
aliiongoza Twiga Stars kwenye fainali za michezo ya Afrika (All Africa
Games) zilizofanyika nchini Congo Brazzavile Septemba mwaka jana, baada
ya kuiondoa timu ya taifa ya Zambia katika hatua ya mtoano.
TFF
imesikitishwa na taarifa za kujiuzulu kwa kocha huyo mwenye leseini A ya
CAF, ambaye amekuwa akizinoa timu za taifa za wanawake ya wakubwa
(Twiga Stars) pamoja na timu ya wanawake wenye umri chini ya miaka ya 20
(Tanzanite) tangu mwaka 2013.
Kufuatia
kujiuzulu kwa kocha Kaijage, TFF inaendelea na programu za maendeleo ya
soka kwa wanawake, ikiwemo kuendesha ligi ya wanawake (Tanzania Women
League).
TFF inamtakia kila la kheri kocha Rogasian Kiajage katika shughuli zake.
Aidha
maandalizi ya mchezo kati ya Twiga Stars dhidi ya Zimbambwe yataendelea
chini ya kocha atakayeteuliwa kuchukua nafasi yake, mchezo utakaochezwa
mwezi Machi mwaka huu na mshindi kucheza na Zambia.
TFF itaendelea kupambania kwenye maendeleo ya soka la wanawake.