Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais
Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Chancellor of
the University of Dar es salaam).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Ikulu Jijini Dar
es Salaam, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 17 Januari, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
21 Januari, 2016.