Ukraine
inatarajia kurejesha kwenye himaya take kuanzia mwaka 2016 udhibiti wa
maeneo yanayoshikiliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.
Ukraine
pia inataka kuunda utaratibu wa kimataifa utakaozishirikisha Brussels na
Washington ili kurejesha kwenye himaya yake eneo la Crimea
lililounganishwa na Urusi, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema
Alhamisi hii.
"Mwaka
2016, uhuru wa Uraine utarejeshwa katika maeneo ya mikoa ya Donetsk na
Lugansk inayosikiliwa na waasi", ambapo vita vimesababisha zaidi ya watu
9,000 kupoteza maisha tangu Aprili mwaka 2014, Bw Poroshenko amesema,
huku akiahidi kutumia tu uwezo wa kisiasa na kidiplomasia kwa
kufanikisha hilo.
Kuhusu
eneo la Crimea lililounganishwa kwa Urusi mwezi Machi 2014, Kiev ina
mpango wa"kupendekeza kuanzisha utaratibu wa kimataifa ili kumaliza hali
hiyo", Rais Poreshenko ameongeza.
Moscow na
Kiev zinaendelea kukabiliwa na mgogoro mkubwa tangu kuingia madarakani
nchini Ukraine kwa mtu anayeungwa mkono na nchi za magharibi mwanzoni
mwa mwaka 2014, na kufuatiwa na kuunganishwa kwa eneo la Crimea kwa
Urusi kufuatia kura ya maoni yenye utata, kisha mgogoro wa kuyatenga na
Ukraine maeneo yanayoshikiliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi,
mashariki mwa Ukraine.