Mheshimiwa Esther Bulaya (mb)
Mbunge
wa jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya aliyekuwa amelazwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Tarime alikokimbizwa Jana Jumapili baada ya
kuzidiwa akiwa mahabusu ya polisi mjini Tarime, amehamishiwa
Hospitali ya Rufaa ya Bugando jjijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Katibu
wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche amesema kuhamishiwa Bugando kwa
mbunge huyo kumewezekana baada ya kupata dhamana ya polisi aliyowekewa
na watu watatu akiwemo wakili wake, Alex Masaba.
Wengine
waliomdhamini kwa kusaini hati ya Sh20 milioni ni Mbunge wa Tarime
mjini Esther Matiko na Mwenyekiti wa Mtaa wa Songambele ‘B’, Pamba
Chacha.
Heche
amesema kabla ya kuachiwa kwa dhamana Mkuu wa Wilaya ya Kipolisi (OCD),
wa Tarime, Thomas Mapuli alimtembelea mbunge huyo hospitalini kuona
hali yake kiafya.