Mbunge
wa Iringa mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa ameibuka
na kumchana Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku na kusema
uelewa wake juu ya hoja za Mwanasheria Tundu Lissu ni mdogo sana.
Msigwa
amesema haya siku moja baada ya Mbunge Msukuma kudai kuwa yeye anaunga
mkono kauli ya serikali kuhusiana na wanasiasa kuchochea sakata la ndege
huku akiwatuhumu kuwa wapinzani wanatafuta kiki na kusema ni waongo
watupu.
"Msukuma
anasukumwa na uelewa Mdogo wa mambo ya kisheria na kimataifa kwa uelewa
wake juu ya hoja za Tundu Lissu ni sawa na kobe kushindana na twiga kwa
uwezo wa kuona Mbali" alisema Peter Msigwa
Aidhaa Mchungaji Msigwa ameitaka serikali kutoa majibu yanayoridhisha kuhusiana na ndege inayoshikiliwa nchini Canada
"Hoja
zilizotolewa na Serikali juu ya kukamatwa kwa ndege yetu huko nchini
Canada Bombadier Q 400 zinafedhehesha Taifa na kuondosha weledi na
umahiri wa Serikali katika kukabiliana na maswala makubwa ya nchi yetu.
Kinachoshangaza Serikali badala ya kujibu hoja kuntu za Mh, Lissu
imeendeleza kufanya mazengaombwe yasioleweka kwa watanzania ikisaidiwa
na Msukuma mbunge wa Geita. Mpaka sasa Serikali haijatoa majibu ya
kuridhisha kuhusiana na sakata hili" alisisitiza Msigwa
Mchungaji Msigwa ameeleza kuwa serikali inapaswa kuja na majibu katika hoja kadhaa ambazo Tundu Lissu aliziibua
"Lissu
anawataja wanasheria wa serikali kutowajibika katika kuishauri serikali
kinyume na taaluma zao . Watu hawa wamekuwa hawana Masada kwa Serikali
wamekuwa wakiingiza mkenge Serikali kila mara na siwashangai kina Prof.
Kabudi , Dr. Mwakyembe mithili ya Dr. Benson Banna ambae kila siku
amekuwa akiidhalilisha taaluma ya wasomi.
"Serikali
mpaka sasa , haijawapa watanzania uhakika ni kwa namna gani mali za
watanzania ikiwemo majengo ya balozi zetu zilizopo nje ya nchi zitakuwa
salama . Watanzania wanataka majibu yenye uhakika juu ya mali zao
kuendelea kunaswa huko nje" alimalizia Peter Msigwa