Rais wa Marekani Donald Trump, wakati akitangaza mkakati mpya kwa Afghanistan Agosti 21, 2017 Fort Myer, Virginia.
Rais wa Marekani Donald Trump amema kuwa mpango wake ulikuwa ni wa
kuondoa vikosi vya Marekani, lakini badala yake ameamua wanajeshi hao
kubakia ili kuzuia kurudia makosa ambayo yalitokea nchini Iraq.
Amesema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan.
“Kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Afghanistan kutawapa nafasi magaidi kujidhatiti vilivyo, ” amesema Bw Trump.
Bw Trump amesisitiza kuwa kitendo cha
Marekani kujiondoa kwa haraka nchini Afghanistan, kitatatoa nafasi kwa
ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea Iraq.
Rais Donald Trump, kupitia Televishen,
amesema akisisitiza kuwa kipaumbele cha Marekani ni kutokomeza mtandao
wa ugaidi na kutekeleza masuala yenye maslahi katika usalama wa taifa la
Afghanistan.
Licha ya kauli hiyo, Bw Trump
hakuzungumzia muda wa mwisho wa ushiriki wa Marekani nchini Afghastan na
idadi kamili ya ongezeko la wanajeshi.
Wakati huo huo rais Donald Trump amilaumu Pakistan kuwahifadhi magaidi, huku akiitaka nchi hiyo kuachana na mpango huo.