Mapema leo asubuhi kumetokea adha ya
usafiri,kufuatia Madereva katika kituo cha mabasi cha simu 2000 Manispaa ya
Ubungo jijini Dar kugoma kutoa huduma ya usafiri,kwa kile walichodai
kupandishiwa tozo kutoka shilingi 500 hadi 1000.
Akizungumza zaidi mmoja wa Madereva wa dala dala katika mgomo huo (hakutaka
kujitambulisha jina),alisema kuwa wao hawawezi kulipa tozo hiyo wakati
miundombinu ya kituo hicho si rafiki na hairidhishi kabisa kwa vyombo
vyao vya usafiri.
"ni vyema wakazirekebisha kwanza changamoto kadhaa zilizopo hapa
kituoni,kisha baadae waje na huo mkakati wao wa kutupandishia hiyo tozo
yao,lakini kwa sasa itakuwa vigumu kulipa kwa sababu kama unavyoona
mazingira yalivyo hapa kituoni",alisema mmoja wa Madereva.
Baadhi ya abiria katika kituo cha simu 2000 wakiwa wamepigwa na butwaa