Mkuu wa Mkoa
Tabora Bw. Aggrey Mwanri ametoa mwezi mmoja kwa mmiliki wa kiwanda cha
Maziwa cha Tabora kuhakikisha anarekebisha kasoro zilizosababisha
kufungwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa mwaka 2016 la sivyo Serikali
itakichukua na kumpa mtu mwingine ili akiendeshe.
Bw. Mwanri alitoa agizo hilo jana mjini Tabora baada ya kutembelea Kiwanda ili kujionea mazingira yaliyosababisha kisimamishwe.
Alisema kuwa mara baada ya kipindi cha
mwezi kukamilika na kama Mmiliki wake atakuwa ajarekebisha mapungufu
aliyoelekezwa na TFDA ayafanyie kazi itabidi apelike mapendekezo katika
Wizara inayohusika na Viwanda ili kikabidhiwe kwa mwekezaji mwingine.
Mkuu wa Mkoa huyo aliongeza sanjari na
kumwagiza alerebishe kasoro pia alimtaka apelike Mkataba wa Ununuzi wa
Kiwanda hicho ili kuona kama anazingatia masharti aliyopewa wakati
akikinua mwaka 1998.
Kwa upande wa Meneja wa Kanda ya
Magharibi wa TFDA Dkt.Edgar Mahundi alisema kuwa walipofanya ukaguzi
katika kiwanda hicho walikuta maziwa yakizalishwa katika mazingira
ambayo ni hatari kwa afya ya watumiaji.
Alisema kuwa wakikuta mrundikano wa maji
machafu kuzunguka Kiwanda na kumwangiza ajenge mtaro wa kuyaondoa
lakini hadi hivi sasa ameshindwa kuujenga.
Dkt. Mahundi aliongeza kuwa jambo
jingine aliagizwa kuhakikisha kuwa anakuwa na maabara na wataalam wa
kutoka katika Kiwanda chake lakini ameshindwa kutekeleza maagizo hayo.
Alisema kuwa TFDA iko tayari kumfungulia
kama atatekeleza maagizo waliompa ambayo yanalenga kulinda afya za
watumiaji wa bidhaa zake.