Mashahidi
wawili akiwemo Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Ofisa wa Polisi, Ramadhan Kingai leo wameieleza Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jinsi Mfanyabiashara Yusuf Manji alivyopelekwa kwa Mkemia
Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.
Mbali
ya Kingai ambaye ni Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ya dawa za
kulevya inayomkabili Manji, Shahidi mwingine ni E.1125 Copro Detective
Sospter.
Mashahidi
hao walitoa ushahidi wao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha
baada ya Wakili Mkuu wa Serikali, Timony Vitalis kueleza kesi hiyo
imeitishwa kwa ajili ya ushahidi.
Akiongozwa
na Wakili Vitalisi, Shahidi Kingai amedai kuwa February 9, 2017 akiwa
Ofisini kwake Central alikuwa na kazi mbalimbali ikiwemo ya kuripotiwa
kwa watuhumiwa wa Dawa za kulevya waliotajwa na RC Makonda.
Amedai
katika watuhumiwa hao alimpokea Yusuf Manji na Askofu wa Kanisa la
Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima baada ya kuripoti wenyewe kituoni
hapo.
“Baada
ya kufika nikiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa dawa za
kulevya nilielekeza Manji na Gwajima wapelekwe kwa Mkemia Mkuu kupimwa,
kwa sababu tuhuma zao ni za dawa za kulevya, ambapo pia walienda
kupekuliwa nyumbani mwao”
Shahidi
huyo akadai kuwa amri ya kupimwa ilitekelezwa na Detective Copro
Sospeter, ambapo baada ya kufanyika uchunguzi akapewa taarifa kwamba
Manji anatumia Dawa za kulevya aina ya Benzodiazepines na Gwajima
hatumii.
“Nikiwa
kama Mpelelezi Mkuu niliichukua ripoti hiyo kisha nilielekeza Manji
afunguliwe jalada la kutumia dawa za kulevya ambapo baada ya kufunguliwa
lilipelekwa kwa DPP”.
Baada
ya kueleza hayo, Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo alimuuliza shahidi
huyo kwa nini dawa za kulevya (Benzodiazepines) alizozitaja Mkemia Mkuu
ni tofauti na zilizotajwa kwenye hati ya Mashtaka (Heroin) ambapo
shahidi huyo alijibu hajui na yeye hakuandaa hati ya mashtaka.
Shahidi
wa pili, Detective Copro Sospeter akiongozwa na Wakili Vitalis alidai
kuwa February 9, 2017 saa 5 asubuhi alikuwa Ofisini na alimpeleka Manji
kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kuchubguzwa.
Alidai kuwa maelezo ya kumpeleka Manji kwa Mkemja aliyapata kwa Kingai, ambapo alimpeleka kwa tuhuma za kutumia dawa za kulevya.
”
Nilimchukua Manji na kumpeleka msalani ili ichukuliwe sampo ya mkojo
wake ufanyiwe uchunguzi, ambapo kuna kielelezo cha fomu kuhusu suala
hilo na naomba kipokelewe na Mahakama.”
Alieleza kuwa baada ya mtuhumiwa kuchunguzwa alichukua majibu kisha alirejeshwa Polisi na taratibu kufatwa.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hadi leo August 23, 2017.