Serikali
imetoa miezi mitatu kwa halmashauri zote nchini kujenga vyumba vya
upasuaji kwenye zahanati na vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi
wanapata huduma za matibabu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis
Kigwangalla amesema Rais John Magufuli alishatoa maelekezo kwa nchi
nzima kuhakikisha zahanati na vituo vya afya,vinakuwa na huduma za
upasuaji.
Dk
Kigwangalla pia ametoa mwezi mmoja kwa halmashauri ya Meru wilayani
Arumeru, kuhakikisha imefunga mifumo ya kielektroniki kwenye zahanati
na vituo vya afya ili kudhibiti upotevu wa mapato.
Amesema Serikali haipo tayari kuona mapato yanaendelea kukusanywa kwa kutumia mfumo wa zamani wa kutumia vitabu.
Amesema lazima
vituo vya afya na zahanati ziwe na mashine za vipimo vya magonjwa, na
upasuaji mdogo lazima ufanyike ili kupunguza msongamano wa wagonjwa
kwenye hospitali za wilaya na mikoa.
"Serikali
ipo katika hatua za kuboresha huduma za afya hivyo lazima kituo cha
afya na zahanati zifanye uchunguzi wa magonjwa na upasuaji," alisema
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Christopher Kazeri,
amesema halmashauri yake, imejipanga kutekeleza maelekezo hayo kabla ya
Desemba mwaka huu.