Wekundu wa Msimbazi Simba SC Jumatano ya jana February 7 2018 walikuwa uwanja wa Taifa DSM kucheza mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC, Simba katika game hiyo walifanikiwa kuibanjua timu ya Azam kuibuka na ushindi wa goli 1-0 likifungwa na 'muhenga' Emmanuel Okwi dakika ya 37.
Goli hilo la Okwi linakuwa ni goli lake la 13 katika Ligi msimu huu akiongoza katika list ya wafungaji hadi sasa, baada ya game hiyo afisa habari wa Simba Haji Manara ametumia ukurasa wake wa instagram kuhoji kuhusiana na wale waliokuwa wanambeza Okwi na kumtania kuwa mhenga.
'Mhenga' Emmanuel Okwi akiumiliki mpira mbele ya mchezaji wa Azam Fc
Lakini pia pamoja na ushindi huo wa Wekundu hao wa Msimbazi,
Kama umeangalia kwa makini mchezo wa ligi kuu kati ya Simba vs Azam uliochezwa Februari 7, 2018 huenda utakuwa umegundua kwamba katika mchezo huo kulikuwa na kikosi cha wachezaji wa Ghana.
Jumla ya wachezaji nane (8) raia wa Ghana walicheza mchezo huo, idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni kuheza kwa pamoja kaika mchezo mmoja.
Mchezo huo ambao ulimalizika kwa Simba kushinda 1-0 dhidi ya Azam, waghana sita walianza kwenye vikosi vya kwanza vya timu hizo. James Kotei na Asante Kwasi walianza kikosi cha kwanza cha Simba huku Razak Abarola, Daniel Amoa, Yakubu Mohamed na Enock Atta-Agyei walikuwa kwenye timu iliyoanza kwa upande wa Azam.
Baadaye Azam walifanya mabadiliko kwa kumuingiza Bernard Arthur (raia wa Ghana) kuhukua nafasi ya Yahya Zayd na Simba walimtoa Emanuel Okwi nafasi yake ikachukuliwa na Nicholas Gyan (raia wa Ghana) ambao walikamilisha idadi ya waghana nane kucheza mechi hiyo.
Kwa sheria na kanuni za soka, zinaruhusu timu kucheza mechi ikiwa na wachezaji wasiopungua saba (idadi ya chini kabisa) lakini pia wasizidi 11 (idadi ya juu zaidi), kwa maana hiyo raia hao wa Ghana wangeunda kikosi chao cha wachezaji nane.
Kikosi cha wacheza wa Ghana waliocheza Simba vs Azam: Razak Abarola, Daniel Amoa, Yakubu Mohamed, Asante Kwasi, James Kotei, Nicholas Gyan, Enock Atta-Agyei, Bernard Arthur. (3-3-1).