Bendi ambayo ilikuwa inakuja kwa kasi ya ajabu hapa chini ya Vibration Sound, Ambayo pia ni bendi mama katika Kampuni ya ASET sasa imevunjwa rasmi na Mkurugenzi wa Aset ambaye pia ndiye mmiliki wa bendi hiyo Asha Baraka.
Amesema kilichompelekea kuifungia bendi hiyo ni UTOVU wa NIDHAMU IKIWA ni pamoja na kwenda kinyume na sheria za kampuni kwani ilifikia hatua wlikuwa wanatumia jina la VIBRATION MUSICA ili kujicha mapato.
Asha amesema ameamua kufunga mpaka hapo atakapopata kundi jingine.
Lakini ameongeza kwamba atakayebakia katika bendi hiyo ni mpiga gitaa maarufu wa bendi hiyo Eliston Angai.
Bendi hiyo ilitesa sana na ngoma zake kali sana kama vile 'mkono kwenye shavu', 'shu shu shu' 'lucky' Pamoja na nyingine kibao.
Mpiga gitaa wa iliyokuwa Vibration Sound Eliston Angai.