Mdau kwa heshima na taadhima yako naomba leo mimi na wewe tujaribu kapanuana mawazo kutokana na hili ambalo mimi nimekutana nalo huko kitaani kwetu tunakoishi kila siku.
Ishu ni kwamba eti, muonekano wa mtu pia unachangiwa sana na mavazi yake.
Mimi nimeumiza sana kichwa changu katika kutafuta ukweli juu ya hilo nikaona hata,! ngoja nije nishee na wewe. Na kwa kutafuta ushahidi nikazama katika laibrari yangu na kuibuka na picha zifuatazo.
Hapo juu ni mimi kaka yenu
a.k.a Master 'E' a.k.a Sana tuu!! nikiwa kunako pozi la ki faza faza zaidi,
Sasa naomba nikuulize swali, je kutokana na hizo picha mbili tofauti wewe umeweza kuitambua tabia yangu?
Hebu angalia na kivazi hicho alichopiga huyo mwanadafada katika picha ya hapo chini
Vipi.! tabia yake umeweza kuijua?
Na hao jamaa wao ni wanamuziki wa bendi deshi deshi ya muziki. Hapo napo vipi.!
Ene wei sio kesi kubwa sana kwani mimi nilikuwa nataka tujaribu kupanuana mawazo mimi na nyie wadau. kama unafikiri una mtazamo chanya zaidi yangu usisite nakukaribisha, nibonyezee katika Email zifuatazo,
e656646@hotmail.com au :
esokone@yahoo.com.