TIMU YA SOKA YA AFRICAN LYON YA DAR ES SALAAM
Kutoka kushoto waliosimama: John Mbugwa, Abdul Masenga, Abu Ubwa, Castory Mumbara, Zuber Ubwa. Waliochuchumaa: Yusuf soka, Sultasn Kittu, Aziz Sibo, Rashid Gumbo Mbwana Samatta and Idrisa Rashid.
Baada ya timu hii kuwatoa jasho mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga leo African Lyon wanashuka katika dimba la uhuru jijini Dar Es salaam kupepetana na timu ya Mtibwa Sugar kutoka kule Manungu Turiani mkoani Morogoro.
Mshambuliaji wa Africa Lyon Idrisa Rashid akimtoka mlinzi wa Yanga, mwishoni mwa wiki katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara. Timu hizo zilitoka suluhu ya kufungana goli 1-1. Mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru jijini Dar Es Salaam.