KINGWENDU NGWENDULILE
MUIGIZAJI NA MCHEKESHAJI MAARUFU NCHINI PENGINE NA HATA KATIKA UKANDA HUU WA AFRIKA MASHARIKI KWA UJUMLA ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA RASHID MWINSHEHE A.K.A ‘KINGWENDU NGWENDULILE’ AMEJIKUTA AKIINGIZWA MJINI NA PROMOTA MMOJA JIJINI MWANZA.
KINGWENDU ALIPOONGEA NA BLOGU HII ALIITONYA KWAMBA, PROMOTA HUYO ‘AMEMPIGA CHANGA LA USO’ KIASI CHA FEDHA SHILINGI MILIONI 1.5 AMBAZO ALIZINYAKA BAADA YA KUPIGA SHOO KULE KANDA YA ZIWA.
KINGWENDU AMESEMA PROMOTA HUYO ANAYEKWENDA KWA JINA LA SAID AMEMFANYIA KITU KIBAYA SANA, KWANI ALIMCHUKUA VIZURI BONGO AKAMPA ADVANCE, KULA, KULALA HAIKUWA NA MATATIZO, JAMBO LILILOFANYA SUPER STAA HUYO AMUAMINI PROMOTA WAKE KUMBE DUUU.!! PROMOTA NI NOMAAA.
KINGWENDU AMENITONYA KAKA YENU KWAMBA “BAADA YA KUPIGA SHOO KWENYE VIJIJI VYA ZALAGULA, KASARATU, NYANANGO NA KANYALA JIJINI MWANZA, NILIKUWA NIMEKUSANYA SHILINGI MILIONI 1.5 KIBINDONI LAKINI JUU KWA JUU NILIPATA ‘DILI’ KWAHIYO NIKAUNGANISHA SHOO.“PROMOTA WANGU ALINIOMBA NIMPE PESA HIZO ILI AKANIWEKEE KWENYE AKAUNTI YANGU, MIMI KWA SABABU NILIKUWA NIMESHAMUAMINI NILIMPA LAKINI HUWEZI KUAMINI, BAADA YA HAPO KILA NIKIMPIGIA SIMU NI STORI TU.
SASA ISHU IKO HIVI WEWE KINGWENDU KWANI BENKI HUPAJUI HADI JAMAA AKUPELEKEE HUO MKWANJA WAKO BENKI?????
Na nyie mapromota feki hiyo sio poa bwanaaaa