Bob Junior.Rais wa ma- sharobaro Bob Junior a.k.a Mr. Chocolate, Amesema kuwa kuna watu wanaomtishia maisha na tayari ameshawachukulia RB inayosomeka: OB/RB/6303/2011. Bob jr amefunguka kuwa watu hao ni Diamond a.k.a the Platnum, Shetta pamoja na meneja wa Shetta anayekwenda kwa jina la Shabaha.
Diamond na Wema Sepetu.
Story ambazo kwa sasa zina 'make headline' ni kwamba mrembo Wema Sepetu alitupwa selo katika kituo cha polisi cha oysterbay baada ya kumpigia simu Bob Jr na kumvurumishia mvua ya matusi na kumtishia kumtumia watu kumlawiti. Bob Jr alifanikiwa kuyarekodi mazungumzo hayo baina yake na Wema Sepetu ambapo ameyatumia kama ushahidi. Lakini kwa sasa Wema yupo nje kwa dhamana.