Bibiciya Mfwengi.
Hii ni siku WMMM walipokuwa jijini Dar na mwanadada Bibiciya Mfwengi alipoawaacha midogo mwaa mashabiki kwa mauno yake
Yule mwanadada aliyewapagawisha wengi kwa uchezaji wake Bibiciya Mfwengi wa Wenge Musica Maison Merre amesemekana kuikacha bendi ya werason na kukimbilia kwa Koffi Olomide alikokuwa mwanzoni.
Akizungumza na Mukwata DMTV Bibiciya amesema kuwa bado hajaamua kuliongelea kiuwazi sana hasa sababu za yeye kuhama lakini kwenye Clip hiyo Bibiciya anaonekana akifanya mazoezi na wanamuziki wa Koffi.
Habari zinasema Werason amekuwa akikimbiwa na wanamuziki wake kwani hata bingwa wa Atalaku/kughani wa bendi hiyo Prince amesemakana kuondoka, si yeye tu bali hata mwanamuziki mwingine mahiri na mtunzi Eboa pia wamesemwa kuondoka kwenye bendi hiyo na Eboa Lotin amesemekana akionekana mara kwa mara na Watu wa Koffi Olomide.
Hivi karibuni kundi la WMMM (Wenge Musica Maison Mere) lilifanya ziara huko Ulaya na mwanamuziki wake mmoja
Olivier alisemekana kubakia nchini Ufaransa ambako alisema kuwa anataka kurudi shule kidogo. Angalia video hii na mahojiano kwa wale wanaofahamu Kifaransa.