Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la #TegetaEscrow.
Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe
madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. Akafanyiwa uchunguzi
na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili.
Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri?
Ameshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?
Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika
Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta
anatetea ubadhirifu. Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa
hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa
1) Azuie kuanzia sasa malipo ya
‘capacity charges’ kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria
kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO
2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na
Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na
afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi;
huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania
3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU
kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya
kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi
wa Prof. Muhongo.
Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani?
Tuache siasa za porojo porojo