TP
Mazembe imeanza na mguu mbaya michuano ya Kombe la Dunia baada ya
kutolewa katika mechi ya kwanza tu kwa kipigo cha mabao 3-0 kutoka kea
Wajapan.
Sanfrecce
Hiroshima ndiyo iliyotoa kipigo hicho kwa TP Mazembe ya DR Congo ambayo
safu yake ya ushambuliaji inaongozwa na WaTanzania Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu.
Kipigo hicho kinafuta ndoto za WaTanzania hao kufika nusu fainali ya michuano hiyo na kukipiga na River Plate ya Argentina.
Wa Japani walianza kupata bao lao la kwanza katika dakika ya 44 kupitia Yusuke Chajima likadumu hadi mapumziko.
Sanfrecce
walipata bao la pili katika dakika ya 56 lililofungwa na Kazuhiko Chiba
akifunga baada ya kuunganisha kona ya Chajima aliyepiga kona iliyozaa
bao la kwanza.
Wakati
Mazembe wakionekana kupambana kubadilisha mambo hasa baada ya Ulimwengu
kuingia katika dakika ya 46, Sanfrecce walifunga bao la tatu katika
dakika ya 78 kupitia Asano aliyeunganisha krosi Mikic.
Adama Traore na Assale, nusura wafunge kutokana na kujaribu vizuri lakini mwisho mambo hayakuwa mazuri kwa Mazembe.
Sasa Sanfrecce Hiroshima inarudi dimbani Desemba 16 kuwavaa mabingwa wa Amerika Kusini River Plate wanaotokea Argentina.
Nusu
fainali nyingine itakuwa siku inayofuata wakati mabingwa wa Ulaya,
Barcelona watakapowavaa Guangzhou, kikosi kinachonolewa na Philipe
Scolari.