
Shehena ya bidhaa mbalimbali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi
ikiwemo vipuri vya magari kutoka nchi tofauti za Pakistan, India na
Ubelgiji zimekamatwa katika bandari bubu ya Kigombe iliyopo wilayani
Muheza wakati zikiingizwa nchini kinyume cha sheria bila kulipiwa
ushuru.
Askari wa jeshi la polisi zaidi ya 100 wakiwa
wamezingira boti zilizotumika kubeba bidhaa hizo ambapo kaimu kamanda
wa polisi mkoani Tanga mratibu mwandamizi wa jeshi polisi Mayala Towo
amesema shehena ya mzigo huo ni pamoja na mafuta ya kupikia kutoka
Ubelgiji, sukari kutoka India na vipuri kutoka nchi za Ulaya.
Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) tawi la
Tanga Bwana amekiri kuwa hali ya ukwepaji wa kodi katika bandari bubu ya
Kigombe ni ya kutisha kwa sababu sehemu kubwa ya bidhaa zinazouzwa
katika maduka mbalimbali katika baadhi ya maduka yaliyopo katika jiji la
Tanga, Muheza na Mkinga zinatoka nje ambazo inadaiwa kuwa zimeingizwa
nchini kinyume cha sheria hatua ambayo imesababisha bidhaa
zinazozalishwa katika viwanda vya ndani kukosa soko.
Kufuatia hatua hiyo kaimu meneja wa forodha mkoa wa Tanga Bwana
Jumbe Magoti amesema wazingatia sheria zilizowekwa katika zoezi la tozo
za faini kisha watataifisha vyombo vilivyotumika katika usafirishaji wa
bidhaa hizo kutoka kisiwani Zanzibar kuingizwa bara bila kulipiwa
ushuru.