Tume ya Uchaguzi ya Uganda, imesema
kuwa shehena ya kwanza ya karatasi za kura za urais na wabunge,
itawasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Entebbe hii leo.
Bila ya kutaja idadi yake, tume hiyo
imesema karatasi hizo zitaletwa na Paarl Media kampuni ya Afrika
Kusini iliyoshinda tenda ya kuchapisha karatasi za uchaguzi mkuu.
Jumla ya wagombea saba wanawania
urais kujaribu kumg'oa madarakani kwa sanduku la kura rais aliye
madarakani Yoweri Museveni katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari
18.