Kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club ambacho kimefanya kweli kule kigalil nchini Rwanda baada ya kuinyuka timu ya Atraco kutoka Ghana kwa Magoli 2-1 katika michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati. Magoli hayo ya watoto wa Rage a.k.a Simba yalifungwa na mchezaji mpya wa kimataifa Robert Ssentongo aliyesajiliwa kutoka Azam Fc na goli la pili likitiwa katika kamba na Mussa Hassan Mgosi ukipend muite 'Mussa Magoli'. Simba imejitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele.